• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 22 September 2016

    Goti lamuweka kando Mbwana



    MAUMIVU ya goti yamemfanya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji kukosa michezo miwili ya Ligi Kuu.
    Samatta ambaye yupo nje kwa wiki sasa aliumia katika mchezo wa kwanza wa Kundi F Europa League dhidi ya Rapid Viena Alhamisi iliyopita kwenye uwanja wa Allianz, Viena, Austria, ambapo KRC Genk ilifungwa mabao 3-2.
    Nahodha huyo wa Taifa Stars amekosa mechi mbili hadi sasa, moja ya Ligi ya Ubelgiji ambayo walifungwa mabao 2-0 na juzi kwenye Kombe la Ligi ya Ubelgiji, na kushinda mabao 4-0 ugenini dhidi ya Eendracht Aalst.
    Samatta tangu ajiunge na KRC Genk Januari mwaka huu akitokea TP Mazembe ya DRC, amecheza michezo 25 ya mashindano yote, 18 msimu uliopita na saba msimu huu, amefunga mabao manane, matatu msimu huu na matano msimu uliopita.
    Katika michezo hiyo 14 alianza na 11 akitokea benchi na Genk watacheza tena Jumapili kucheza na Kortrijk Uwanja wa Guldensporen mjini Kortrijk kwenye mchezo wa Ligi ya Ubelgiji na Alhamisi wiki ijayo watacheza Europa League watakapoikaribisha Sassuolo ya Italia katika mchezo wa pili wa Kundi F.
    Wakati huo huo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu anayecheza TP Mazembe ya DRC amesema atafurahi endapo timu yake itatwaa Kombe la Shirikisho Afrika.
    Ulimwengu ambaye timu yake mwaka jana ilitwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika, aliyasema hayo Dar es Salaam ambapo yupo akishughulikia pasi yake ya kusafiria ambayo ilikuwa imekwisha na kushindwa kwenda Tunisia.
    “Matokeo ya sare ya ugenini kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza ugenini siyo mabaya ninaamini sasa tutashinda nyumbani na kwenda fainali”, alisema Ulimwengu.
    Mazembe ilitoka sare ya 1-1 na Etoile du Sahel, mchezo uliochezwa Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse, Tunisia Jumamosi iliyopita.
    Mazembe watahitaji sare ya 0-0 katika mchezo wa marudiano nyumbani Septemba 25 ili kwenda fainali, ambako watakutana na mshindi wa jumla kati ya Mouloudia Olympique Bejaia ya Algeria na FUS Rabat ya Morocco.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI