• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 16 September 2016

    Serikali yasomesha nje 159



    JUMLA ya wanafunzi 159 wamepelekwa kusoma nje ya nchi na serikali katika mwaka wa fedha wa 2015/ 2016.
    Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Stella Manyanya amesema wanafunzi hao walikwenda kusoma katika nchi za China, Algeria, Urusi, Misri na Uingereza kupitia Jumuiya ya Madola.
    Manyanya alibainisha hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Tauhida Galloss(CCM) aliyetaka kufahamu bajeti ya mwaka 2015/2016 serikali ilipeleka wanafunzi wangapi kusoma nje ya nchi na kada gani ambazo zilipewa kipaumbele.
    Akijibu swali hilo, Manyanya alisema katika mwaka huo wa fedha serikali ilipeleka wanafunzi 159 na kuzitaja nchi hizo na idadi ya wanafunzi kuwa ni China (84), Algeria (57), Urusi (4), Misri (2) na Uingereza kupitia Jumuiya ya Madola (12).
    Manyanya alisema serikali imekuwa ikipeleka wanafunzi nje ya nchi kwa kuzingatia vipaumbele vya taifa ambavyo ni masomo ya sayansi, teknolojia na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).
    Alisema wanafunzi wanaopelekwa nje ya nchi husoma Shahada ya kwanza, Uzamili na Uzamivu katika fani za Nishati na Madini. Manyanya alitoa mfano wa fani zinazopewa kipaumbele kuwa ni masuala ya gesi na mafuta, mazingira na mabadiliko ya tabia nchi, uhandisi, afya na sayansi shirikishi, usanifu majengo, elimu, uchumi na mawasiliano.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI