WADAIWA sugu wa mikopo ya Elimu ya Juu, wameendelea kumiminika katika ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB) huku ikiripotiwa mpaka sasa tayari wadaiwa 42,000 wameshalipa.
Akizungumza jana katika ofisi za HESLB zilizopo Mwenge Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi msaidizi wa Bodi hiyo Abdul Ally alisema kuwa, tangu walipotoa siku 30 za wadaiwa sigu kuhakikisha wanaanza kulipa madeni hayo, muitikio umekuwa mkubwa.
‘’Kwa siku tunapokea wadaiwa 1200 hadi 1500, hivyo nawaomba wadaiwa wengine waendelee kuja kulipa madenia hayo kwani vinginevyo sheria itachukua mkondo wake’’, alisema.
Wakati huo huo Ally alitaja mabadiliko ya sheria ya mikopo ya HESLB kuwa, kwa sasa makato kwa wadaiwa walioko katika ajira rasmi itakuwa asilimia 15, badala ya 8 kama ilivyokuwa mwanzo.
Ally alisema kuwa makato ya asilimia 15 ni wale waliokuwa katika mfumo wa ajira rasmi, lakini kwa wale ambao hawako katika mfumo huo asilimia 10 ya kipato anachopata kwa mwezi.
No comments:
Post a Comment