• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 6 January 2017

    MAKAMU WA RAIS AFANIKIWA KUINGIZA TANZANIA KATIKA MPANGO WA BIASHARA WA CHINA WA ONE BELT ONE ROAD

    miko
     mikoMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wenyeviti wa TPSF,CTi,TCCIA na ZNCCIA juu ya mpango wa kibiashara unaojulikana kama China One Belt, One Road ulio asisiwa na serikali ya China na unajumuisha bara la Asia, Mashariki ya Kati,Ulaya na Afrika, Ikulu jijini Dar es Salaam.

     Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
    Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Wenyeviti wa TPSF,CTi,TCCIA na ZNCCIA juu ya
    mpango wa kibiashara unaojulikana kama China One Belt, One Road ulio
    asisiwa na serikali ya China na unajumuisha bara la Asia, Mashariki ya
    Kati,Ulaya na Afrika.

    ……………………………………………………………..
    Jitihada za Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan za
    kuiingiza Tanzania katika mpango mkubwa wa Biashara kwenye bara la Asia, Mashariki ya kati,Ulaya na Afrika  umefanikiwa
    baada ya Tanzania kuchaguliwa kuwa miongoni mwa nchi Saba kuingizwa katika mpango unaojulikana kama China One Belt, One Road Stratergy.
     

    Nchi nyingine ambazo zimechanguliwa kuingizwa kwenye mpango huo ni Malaysia,Sri
    lanka, Nepal, Bangladesh,Pakistan na Thailand.


    Baada ya Tanzania kuingizwa rasmi katika mpango huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
    Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye pia Mjumbe katika jopo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kumuwezesha mwanamke kiuchumi akiwakilisha nchi za ukanda wa Kusini na Mashariki mwa Afrika amekutana na Watendaji kutoka
    Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF),Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Biashara (TCCIA) na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kuwaeleza kuhusu muhimu wa Tanzania kuingizwa kwenye mpango huo.
     
     


    Makamu wa
    Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania imepata uanachama wa mpango huo baada
    ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mfanyabiashara wa Madini na Vito kutoka
    China Dkt Helen Lau kuhusu manufaa ya mpango huo na Makamu wa Rais alimwomba
    Mfanyabiashara huyo kuisaidia Tanzania kuingia kwenye mpango huo China One
    Belt, One Road Stratergy jambo ambalo limefanikiwa.


    Makamu wa Rais
    Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa Mwezi Septemba mwaka 2016 ulifanyika mkutano
    Guangdong nchini China kujadili maombi ya kujiunga na mpango huo ambapo Makamu
    wa Rais alimwomba Dkt Helen kuiwakilisha Tanzania katika kuwasilisha maombi na
    kwa bahati nzuri ombi la Tanzania lilikubaliwa na kupata uanachama katika
    mpango huo mkubwa wa China One Belt, One
    Road.


     


    Makamu wa
    Rais amesema kuwa moja ya fursa zinazotolewa na Serikali ya China katika mpango
    huo ni kila nchi Mwanachama kupewa vyumba vya ofisi katika jengo linaloitwa 21st
    Century Maritime Silk Road Expo bila kulipa kodi ya pango kwa miaka Mitatu na
    baadhi ya vyumba vya jengo hilo vitatumiwa na nchi husika kuonyesha na kutangaza
    bidhaa zao.


    Kufutia
    Tanzania kuingizwa kwenye mpango, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewaagiza
    watendaji wa sekta binafsi alikutana nao ikulu jijini Dar es Salaam wajipange
    na kuweka mikakati ya namna ya kunufaika na mpango huo haraka iwezekanavyo.
     
     
    Amesisitiza kuwa mpango huo wa China One
    Belt, One Road Stratergy uliobuniwa na serikali ya China kwa dhamira ya
    kuzikutanisha Jumuiya za Wafanyabiashara za  Mashariki mwa bara Asia, Mashariki ya kati,
    Ulaya na Afrika kwa ajili ya kubadilishana mawazo,kuonesha njia na kupeana
    ushauri wa jinsi ya kukuza biashara kati ya nchi wanachama wa mpango huo kwa
    lengo la kuiwezesha sekta ya biashara kuchangia nyema kwenye uchumi wa mataifa
    yao.

    Makamu wa
    Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania baada ya kuingia kwenye mpango huo itanufaika
    na fedha za mfuko kwa ajili ya maendeleo ya miundombinu ambazo zinatolewa kwa
    nchi zilizojiunga na mpango huo.
     
     

    Kwa upande
    wake, Mweyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania Godfrey Simbeye na Mwenyekiti
    wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar Taufik Turki wamemuahidi
    Makamu wa Rais kuwa watatumia fursa hiyo ipasavyo ili kukuza biashara kati ya
    Tanzaniana Nchi wanachama wa mpango huo.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI