Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema atamuagiza Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) kuchunguza ukusanyaji mapato ya Shirika
la Ndege Tanzania(ATCL)
Ameyasema hayo mapema hii leo alipotembelea Makao Makuu ya shirika
hilo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujionea mwenendo wa uendeshaji
wake.
“Nitamuagiza CAG aje aangalie mwenendo wa ukusanyaji wa mapato ya
shirika hili kuanzia mwaka jana lilipoanza kufanya kazi hadi sasa,”
amesema Majaliwa.
Amesema kuwa Serikali haiko tayari kuona shirika hilo linakufa tena,
hivyo amewataka viongozi wake wahakikishe linaendeshwa kwa mafanikio kwa
manufaa ya Taifa.
Pia amewataka waache kukusanya mapato kwa kutumia risiti za kuandika
kwa mkono na badala yake waanze kutumia mfumo wa kieletroniki ili
kuzuia upotevu wa mapato hayo.
Katika hatua nyinginre, Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa
Fedha na Utawala, Witness Mbaga ajiridhishe na fedha zinazokusanywa
katika eneo la mizigo kama ziko sahihi, lengo ni kudhibiti upotevu wa
mapato.
Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka viongozi wa shirika hilo kuhakikisha
wanazingatia ratiba ya njia na muda wa safari ili wasipoteze watej

No comments:
Post a Comment