Kupitia kikao cha baraza la madiwani la Halmashauri
ya Ilala Mstahiki Meya Charles Kuyeko amehaidi kufanya kikao maalum
kwaajili ya kuzungumzia miradi ya Halmashauri hiyo ili waweze kukusanya
mapato yenye tija kwa Halmashauri hiyo.

Kauli hiyo ya mstahiki meya imekuja kufuatia mchango wa
mbunge wa jimbo la Segerea Bonnah Kaluwa kuitaka Halmashauri kuweka
utaratibu utakao walinda bodaboda licha ya kuwafanya wao ndiyo chanzo
cha mapato, ukizingatia serikali imesitisha ajira kwa sasa.

Katika hatua nyingine baraza hilo limezungumzia matokeo
mabovu ya kidato cha nne kwa shule za Mbondole, Kitonga na Nyeburu
ambapo Mbunge wa jimbo la Ukonga Mwita Waitara amezitaja sababu za
miundombinu ndiyo iliyopelekea wanafunzi wa shule hizo kufeli kwani zipo
mbali na wanafunzi wengi wanao soma hapo, sababu inayopelekea wengi
kutokwenda shule kwa kukosa nauli, kwakuwa usafiri mkubwa unatumika ni
bodaboda kutokana na miundombinu isiyo rafiki.

Pia Mbunge huyo amewataka wazazi kutoichukulia vibaya dhana
ya elimu bure kwa kuitupia mzigo serikali kwani nao wanapaswa kushiriki
kwenye shughuli za maendeleo ya elimu ikiwemo kuchangia ujenzi wa uzio
na mambo yenye tija kama hayo.

No comments:
Post a Comment