Baada ya kuja na operesheni ya kupambana
na dawa za kulevya, jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
linaweza kuwa ndilo lililotajwa zaidi katika mkutano wa Bunge
uliomalizika wiki iliyopita na kwenye mitandao ya kijamii kwa wiki ya
pili sasa.
Makonda alianza kuwa mjadala ndani na nje
ya nchi baada ya kutaja orodha ya kwanza na ya pili ya watu maarufu
wakiwamo wasanii, wanasiasa na viongozi wa dini na kuagiza wafike Kituo
Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam wahojiwe kuhusu dawa za kulevya.
Kasi ya kutajwa kwa jina lake iliongezeka
zaidi Jumatano iliyopita baada ya kumtaja Kiongozi wa Kambi Rasmi ya
Upinzani bungeni, Freeman Mbowe, Askofu Josephat Gwajima na
mfanyabiashara Yusuf Manji.
Hata hivyo, Mbowe, Gwajima na Manji
wamekanusha vikali kuhusika na biashara hizo na kuahidi kumshtaki
Makonda kwa kashfa. Gwajima na Manji wameshahojiwa polisi.
Katika mtandao wa kijamii wa JamiiForums,
hadi kufikia juzi saa 8:00 mchana, kulikuwa na kurasa 49 ambazo jina la
Makonda lilikuwa limetajwa mara 961 katika mijadala iliyokuwa
ikiendelea.
Mijadala hiyo ilikuwa ikihusu kama
Makonda yuko sahihi au la katika utaratibu alioutumia na kama ana
mamlaka ya kuagiza watu kuripoti polisi.
No comments:
Post a Comment