Mkurugenzi wa Habari na Msemaji
Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas akizungumza na Maafisa Habari na
Tehama wakati wa Mafunzo elekezi ya matumizi ya tovuti katika Mikoa na
Halmashauri za Wilaya nchini yaliyofadhiliwa na Shirika la Misaada la
Marekaani (USAID) na kusimamiwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo na Wakala ya Serikali Mtandao. Mafunzo hayo yalianza tarehe
9-20 Februari, 2017,
…………………………………………………………….
Na Ismail Ngayong- MAELEZO- Mwanza
MAAFISA Habari na Mawasiliano katika sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Wilaya nchini wametakiwa
kujitokeza na kuwajibika kikamilifu ili kuwawezesha waaajiri wao
kutambua wajibu na majukumu yao ya msingi katika kutangaza shughuli na
mafanikio ya Serikali katika maeneo yao ya kazi.
Rai hiyo imetolewa leo Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas
wakati alipokuwa akizungumza na Maafisa Habari na TEHAMA katika mafunzo
elekezi ya tovuti yanayofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani
(USAID) na kusimamiwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
pamoja na Wakala ya Serikali Mtandao (EGA).
Kwa
Mujibu wa Dkt. Abbas alisema katika ulimwengu wa sasa suala la
teknolojia ni jambo lisiloupekika, hivyo ni wajibu wa Afisa Habari
kutmia nyenzo za kisasa za mawasiliano ikiwemo tovuti ili kuhakikisha
kuwa wananchi na wadau wa maendeleo wanapata taarifa sahihi na
zilizozingatia wakati.
“Zipo
taarifa za miradi mbalimbali ambayo Serikali imeifanya, pamoja na
taarifa za bajeti za halmashauri ambazo wananchi watanapenda kuzifahamu,
hivyo ni wajibu wenu Maafisa Habari kuweka taarifa hizi” alisema Dkt.
Abbas.
Aidha
aliongeza kuwa ni wajibu wa kila Afisa Habari aliyopo katika Mkoa na
Halmashauri nchini aweze kujiwekea malengo ya utekelezaji ili aweze
kujitafakari kwa kuwa kuwa kupitia malengo hayo ataweza kutatua
changamoto mbalimbali zinazomkabili katika eneo lake la kazi.
Akifafanua zaidi Dkt Abbas alisema ili kufikia malengo hayo Maafisa Habari Habari hawana budi kutengeneza mtandao wa mawasiliano baina yao ili kuwawezesha kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi.
Dkt.
Abbas alisema Serikali inatambua changamoto mbalimbali zinazowakabili
maafisa Habari katika maeneo yo ya kazi, ambapo baadhi ya changamoto
hizo zimeanza kupatiwa ufumbuzi ikiwemo suala la miongozo ya majukumu ya
Afisa Habari na Mawasiliano.
Kwa
Upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Ofisi ya
Rais- TAMISEMI, Rebbeca Kwandu alisema katika mafunzo hayo yaliyotolewa
kwa Maafisa Habari na TEHAMA yatasaidia kwa kiasi kikubwa kujibu hoja
na kero mbalimbali za wananchi ambazo zimekuwa zikiwasilishwa mara kwa
mara katika halmashauri mbalimbali nchini.
“Afisa Habari atakuwa ndiye mhusika wa karibu zaidi atayekuwa
akiweka maudhui ya tovti hizi lakini pia Afisa TEHAMA yeye atawajibika
kwa kiasi kikubwa katika eneo la la ufundii” alisema Kwandu.
No comments:
Post a Comment