Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema
amezindua WiFi ya mtandao wa bure kwa katika chuo cha elimu ya biashara
(CBE) kampasi ya Dar es Salaam, na kuwaomba wanafunzi wa chuo hicho
kuitumia WiFi hiyo kwa tija ya masomo ikiwemo kufanya tafiti mbalimbali
zitakazo wasaidia katika masomo yao na jamii kwa ujumla.
DC
Mjema ameupongeza mradi huo wa WiFi ya bure ambao unaendeshwa na
kampuni ya Tanzanite Technology Co. Ltd kwa kushirikiana na manispaa ya
Ilala na kampuni ya simu ya TTCL kwani unataraji kuwanufaisha zaidi ya
watumiaji 7000 ambao ni wahadhili, wafanyakazi, wanachuo na wadau
mbalimbali.
Huku lengo kubwa likiwa ni kujenga
daraja la Teknolojia na kuondoa pengo kati ya walio na uwezo wa kutumia
mtandao wa Internet na wasio kuwa na uwezo, ambapo DC Mjema amesisitiza
endapo kutakuwa na matumizi sahihi ya Teknolojia hiyo taifa kwa ujumla
litapiga hatua na ufaulu kuongozeka kwa wanafunzi nchini.



No comments:
Post a Comment