• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 6 April 2017

    Majibu ya bosi wa Tongwe Records kuhusu kukamatwa kwa Roma

    April 5 2017 kulikuwa na taarifa ambazo zilikuwa zinadai staa wa Hip Hop Bongo Roma mkatoliki kukamatwa na watu wasiojulikana jambo lililoibua hisia za watu mbalimbali wakiwepo mastaa wa Bongo Fleva na wanasiasa.
    Leo April 6 2017 millardayo.com imemtafuta mmiliki wa Tongwe Records J. Murder ili kujua kama taarifa hizo ni kweli na kitu gani kinaendelea ambapo aliyasema haya…>>>“Ni kweli jana mida ya saa moja walikuja watu ambao hawajulikani wametokea wapi, wakaniulizia mimi pamoja na Roma japo mimi hawakunipata. Ikabidi wamuhoji Roma na wakaingia studio wakachua baadhi ya vitu na kuwachukua baadhi ya watu na kuondoka nao.
    “Amechukuliwa Roma, Moni, Bello na kijana wa kazi wa mama yangu anaitwa Emma na hatujui wako wapi na wanahojiwa kitu gani, ila mpaka sasa napokea simu nyingi zikiwaulizia ndugu zao wako wapi, lakini mimi hadi sasa hivi sijui Roma yupo wapi.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI