Rapper huyo amekiambia kipindi cha On The Eight cha ETV, msanii yoyote ambaye wimbo wake umepokelewa vizuri basi atapewa nafasi zaidi kwa kipindi hicho hata kwa kuachia albamu ili kuwafurahisha zaidi mashabiki wao.
Temba ameongeza kuwa hata wazo la kuanzisha kituo cha Mkubwa na Wanawe lilianzia kwake kutokana na matatizo kadhaa yaliyowahi kujitokeza huko nyuma kwa baadhi ya wasanii wenzao kujitoa kwenye kundi kwa madai walikuwa wanadhulumiwa na Said Fella.
Kwa sasa Temba na Chege wanafanya vizuri na wimbo wao mpya ‘Go Down’ ambapo video yake mpaka sasa imeshatazamwa mara 533k kwenye mtandao wa Youtube
No comments:
Post a Comment