Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango Bw.Dotto James akibadilishana mkataba wa kibajeti na Balozi wa
Umoja wa Ulaya (EU) nchini Bw.Roeland van de Geer mara baada ya kusaini
mkataba huo Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU)
nchini Bw.Roeland van de Geer akizungumza jambo na waandishi wa habari
juu ya msaada wa shilingi bilioni 486.9 uliotolewa na umoja huo kwa
Serikali ya Tanzania ili kusaidia Bajeti.Kulia kwake ni Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Dotto James.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango Bw.Dotto James akitoa ufafanuzi kwa wahandishi wa habari juu ya
msaada wa shilingi bilioni 486.9 ambao Serikali imeupata kutoka umoja wa
ulaya (EU) kwa ajili ya kusaidia Bajeti.Kushoto kwake ni Balozi wa
Umoja wa Ulaya (EU) nchini Bw.Roeland van de Geer.
Serikali kupitia Wizara ya Fedha
na Mipango imesaini msaada wa shilingi Bilioni 490 usiokuwa na masharti
yeyote kutoka Umoja wa Ulaya ikiwa ni msaada wa kibajeti kwa kipindi cha
miaka minne kuanzia mwaka wa bajeti wa 2017/18.
Mkataba huo umesainiwa na Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James kwa niaba ya Serikali na
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Bw.Roeland van de Geer kwa niaba ya
Umoja wa Ulaya.
Akizungumza na waandishi wa habari
mara baada ya kusaini mkataba huo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango Dotto James amesema Umoja wa Ulaya umetoa msaada huo kutokana na
kuvutiwa na juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika maeneo
mbalimbali ikiwemo kupambana na rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.
“Nadhani mmeshuhudia utiaji saini
huu ulioisha hivi punde na Umoja wa Ulaya wametuhakikishia kuendelea
kutusaidia katika masuala ya misaada ya kibajeti pamoja na kuwa bega kwa
bega na Serikali katika masuala mbalimbali ya maendeleo”,Aliongeza
Katibu Mkuu huyo.
Pamoja na hayo mpango wa pili wa
maendeleo wa Taifa wa Bajeti ya mwaka 2017/18 pia utapewa msaada na
umoja huo kwani wameuona mpango huo una tija na kuweka mkazo katika
viwanda na kilimo.
Kwa upande wake Balozi wa Umoja wa
Ulaya (EU) nchini Roeland Van de Geer amesema kuwa wameliangalia zaidi
suala la utawala kama eneo kuu katika mpango wa ushirikiano na Tanzania
na vilevile wanatazamia maendeleo zaidi katika maeneo ya kilimo,ujenzi
wa barabara za vijijini na nishati.
“Mkataba ambao tumeusaini
utaiwezesha Wizara ya Fedha na Mipango katika ukusanyaji wa
mapato,zitaboresha uwajibikaji na utumiaji mzuri wa mali za Serikali, na
Umoja wa Ulaya unasapoti azma ya viwanda ya Serikali ya Awamu ya
Tano,”Aliongeza Roeland Van de Geer.
Amesema kuwa ushirikiano uliopo
katika ya Tanzia na Umoja wa Ulaya ni mpana sana na utaendelea kuimarika
zaidi katika kipindi hiki ambacho mageuzi ya sera yanahitajika
No comments:
Post a Comment