Askofu Shoo ametoa kauli hiyo, wakati akitoa mahubiri ya ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini.
“Mungu amekupa roho hiyo ya kutokuwa na hofu yakutaja majipu , na majipu haya wewe kwa ujasiri kabisa umesema lazima tuyatumbue kama tunataka kuendelea kama Taifa. Watanzania tulio na nia njema Rais Magufuli tunakuelewa,” alisema Askofu Shoo.
“Sisi kanisa tunakuombea na tuntaendelea kukuombea, uzidi kuwa na ujasiri huo, tunazidi kukuombea kwa Mungu akupe afya njema usiache kusimama katika lile la kweli, na wewe mwenyewe umesema msema kweli mpenzi wa Mungu, endelea kuwa mpenzi wa Mungu Muheshimiwa Magufuli. Tunamuomba Mungu azidi kukupa washauri wema wasio na unafiki, wasio na hila na malengo ya kujinufaisha binafsi
No comments:
Post a Comment