Rais Magufuli ametoa kauli hiyo alipokuwa katika jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro ambapo wananchi wa eneo hilo walishika majani ya kijani ambayo ni ishara ambayo hupelekewa mtu uliyemkosea ukiwa unaomba yaishe.
“Nawashukuru sana wote mliokuja na haya majani ya mti. Nafahamu maana yake na mimi nimewasamehe wote. Najua na ninyi mmenisamehe wote,”alisema Rais Magufuli huku akishangiliwa.
“Tushikamane kwa pamoja tujenge nchi yetu. Hakuna Mtanzania anayekula vyama, Mtanzania anataka maendeleo, anataka hospitali, barabara, anataka madawa, maji yapatikane umeme,”aliongeza Rais Magufuli.
Jumatatu hii Rais Magufuli bado yupo mkoani humo kwaajili ya sherehe ya wafanyakazi ‘Mei Mosi’ ambapo yeye atakuwa mgeni rasmi.
No comments:
Post a Comment