• Breaking News

    ..

    ..

    Friday 23 June 2017

    Idara ya Habari (MAELEZO) Yapokea Kamusi Kuu Kuenzi Kiswahili

    Displaying PIX0.jpg: Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Kamusi Kuu ya Kiswahili toleo la pili kwa Maafisa Habari wa Idara hiyo leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi huyo amenunua Kamusi hizo ili kuwajengea uwezo maafisa hao kutumia maneno sahihi ya lugha ya Kiswahili kama njia ya kuhamasisha matumizi sahihi ya lugha hiyo, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Sehemu ya Huduma za Habari na Picha, Bw. Rodney Thadeus.
    Displaying PIX1.jpg Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya hiyo Sehemu ya Huduma za Habari na Picha, Bw. Rodney Thadeus wakionyesha nakala za Kamusi Kuu ya Kiswahili toleo la pili kwa Maafisa Habari wa Idara hiyo (hawapo pichani) mara baada ya makabidhiano ya Kamusi hizoyaliyofanyika katika Ofisi za Idara hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kamusi hizo zimekabidhiwa na Dkt. Abbasi kwa lengo la kuwajengea uwezo Maafisa hao katika matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili.
    Displaying PIX2.jpg: Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya hiyo, Sehemu ya Huduma za Habari na Picha, Bw. Rodney Thadeus wakisoma nakala za Kamusi Kuu ya Kiswahili toleo la pili mbele ya Maafisa Habari wa Idara hiyo (hawapo pichani) mara baada ya makabidhiano ya Kamusi hizo yaliyofanyika katika Ofisi za Idara hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kamusi hizo zimekabidhiwa na Dkt. Abbasi kwa lengo la kuwajengea uwezo Maafisa hao katika matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili.
    Displaying PIX3.jpg Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari(MAELEZO), Sehemu ya Huduma za Habari na Picha, Bw. Rodney Thadeus akiwasisitizia Maafisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) kutumia Kamusi Kuu ya Kiswahili toleo la pili alizokabidhiwa na Mkurugenzi wa Idara ya hiyo Dkt. Hassan Abbasi leo Jijini Dar es Salaam ikiwa ni njia ya kuhamasisha matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili.Displaying PIX4.jpg
    Picha zote na: Frank Shija - MAELEZO

    Na. Lilian Lundo - MAELEZO
    Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi leo amekabidhi Kamusi Kuu ya Kiswahili kwa watumishi wa Idara ya Habari (MAELEZO) katika ofisi za Idara hiyo zilizopo Jijini, Dar es Salaam.
    Dkt. Abbasi amesema mojawapo ya jukumu la idara hiyo ni kuhabarisha Umma, hivyo kamusi hiyo itakuwa msaada mkubwa katika uandishi wa habari za kila siku.
    “Kamusi hii ina maneno mpaka yaliyoaanza kutumika hivi karibuni, kama vile bajaji. Pia ina misamiati mingi ambayo haitumiki, hivyo kwa kuitumia kamusi hii kutaongeza idadi ya misamiati ya Kiswahili kwa watumiaji wa lugha ya Kiswahili,” amesema Dkt. Abbasi.
    Ameitaka Idara ya Habari kuitumia Kamusi hiyo kama nyenzo muhimu katika kutangaza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi pamoja na kutumia misamiati mipya.
    Hata hivyo, Dkt. Abbasi alitoa ufafanuzi wa neno Mbashara kuwa ndio neno sahihi lenye maana ya inayorushwa hewani moja kwa moja au kuonwa kwa wakati huohuo kupitia redio na televisheni na sio Mubashara kama ambavyo limekuwa likitumika na vyombo vingi vya habari.
    Aidha alitoa mfano wa misamiati mingine iliyopo katika kamusi hiyo kuwa ni neno sharubati linalomaanisha kinywaji laini ambacho hutengenezwa kwa maji ya matunda au sukari na kisha kutiwa rangi. Neno lingine ni mnyange ambalo linamaana ya mtu mwenye mwonekano mzuri, maridadi, mtanashati, mrembo, mlimbwende.
    Dkt. Abbas amewataka watumishi wa idara hiyo kuwa chemchem ya kutumia misamiati iliyoko katika kamusi hiyo ili kukuza lugha ya Kiswahili.
    Kamusi Kuu ya Kiswahili ilizinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Juni 19, mwaka huu, Bungeni Mjini Dodoma.


    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI