Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP
Simon Sirro akipiga saluti wakati wa paredi ya polisi iliyoandaliwa
lililoandaliwa kwa ajili yake kulikagua mapema leo kwenye viwanja vya
kambi ya FFU mjini hapa.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini
IGP Simon Sirro akikagua baadhi ya askari wa jeshi la polisi mjini
Singida leo piga saluti wakati wa paredi ya polisi iliyoandaliwa
lililoandaliwa kwa ajili yake kulikagua.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP
Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada kukagua
askari polisi waliokuwa kwenye paredi kwenye viwanja vya kambi ya FFU
mjini hapa.
………………………….
Picha/Habari na Gasper Andrew.
Mkuu
wa Jeshi la polisi nchini (IGP), Simon Sirro amelipongeza jeshi la
polisi Mkoani Singida kwa juhudi zake za kupunguza matukio ya uhalifu
yakiwemo ya utekeji wa magari kwa kiwango kikumbwa.
IGP
Siro ametoa pongezi hizo leo asubuhi alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari kweye viwanja vya kambi ya kikosi cha kuzuia fujo
(FFU) mjini hapa.
Amesema matukio
ya uhalifu mbalimbali mkoani Singida yamekupungua kwa kiwango kikubwa
kwa sasa, ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
“Hatua
hii inachangia uwepo wa amani na utulivu kwa wananchi wa mkoa wa
Singida hivyo kutoa fursa kuweza kujiletea maendeleo yao ya mkoa
na taifa kwa ujumla” amesema.
IGP
Siro amesema mafanikio hayo yamechangiwa na wananchi kwa kiwanngo
kikubwa kwa kutoa ushuirikiano kwa jeshi la polisi.
Akifafanua
amesema wananchi wamekuwa wakitoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa
jeshi la polisi pindi wanapobaini dalili ama matukio ya kihalifu.
“Kwa
sasa kwa kweli wananchi hata ninyi waandishi wa habari mnatupa
ushirikiano mzuri sana. Ushirikiano huu unachangia kazi zetu kuwa
nyepesi na za mafanikio makubwa. Sasa hivi kule Kibiti mkoani Pwani,
wananchi wanatusaidia mno taarifa zinazohusu mauaji ya watu
wasiokuwa na hatia”, amefafanua zaidi.
IGP
Siro amesema kwa sasa Tanzania inaonewa wivu na nchi jirani kwa namna
tulivyo dhibiti matukio ya kihalifu na kupelekea nchi kuendelea
kudumisha amani na utulivu.
Wakati
huo huo, Mkuu huyo wa jeshi la polisi ametumia fursa hiyo kuwaomba
wananchi waendelee kushirikiana na jeshi hilo, kufichua baadhi ya
watu wanaojihusisha na matukio mbalimbali ya kihalifu ili waweze
kuchukulia hatua stahiki
No comments:
Post a Comment