DHUL- HIJJAH
1) Siku ya kwanza
Nabii Adam (as) alisamehewa makosa yake, Allah atamsamehe madhambi ya atayefunga siku hiyo..
2) Siku ya pili
Nabii Yunus (as) alikubaliwa maombi yake na Allah ya kumtoa ndani ya tumbo la samaki chewa, mwenye kufunga siku hiyo ni kama aliyefanya ibada ya mwaka mzima pasi na kufanya makosa..
3) Siku ya tatu
Ni siku ambayo Allah (SWT) aliitika dua ya Nabii Zakariyya ya kumpa mtoto mwema Nabii Yahya, mwenye kufunga siku hiyo Allah (SWT) ataitika dua yake..
4) Siku ya nne
Ni siku ambayo alizaliwa Nabii Issa (as), mwenye kufunga siku hiyo Allah (SWT) humuondolea matatizo na umaskini..
5) Siku ya tano
Ni siku ambayo alizaliwa Nabii Musa (as), mwenye kufunga siku hiyo Allah (SWT) humtakasa na unafiki na humuondolea adhabu za kaburi..
6) Siku ya sita
Ni siku ambayo Allah (SWT) alimfunulia yeye Nabii Muhammad (saw) kheir, mwenye kufunga siku hiyo hutizamwa kwa jicho la huruma na humlinda na adhabu zake siku ya Qiyyammah..
7) Siku ya saba
Ni siku ambayo milango ya moto wa Jahannam hufungwa na haifunguliwi mpaka siku kumi yatimie, mwenye kufunga siku hiyo Allah (SWT) humfungia milango 30 ya mambo mazito na humfungulia milango 30 ya mepesi..
8) Siku ya nane
Ni siku iitwayo "Tar-wiya", mwenye kufunga siku hiyo hupata malipo ambayo hapana ayajuae isipokuwa Allah (SWT)...
9) Siku ya tisa
Ni siku iitwayo "ARAFAH", mwenye kufunga siku hiyo hufutiwa madhambi ya mwaka uliotangulia na mwaka ijayo
Fanya bidii siku hii kusoma surah
ikhlaas 1000x , Istighfaar 300x , Salatun Nabii 500x na kuzidi, nuia mahitaji yake na inshaa Allah, Allah (SWT) atakukidhia biidhniLah
10) Siku ya kumi
Ni siku ya kuchinja, mwenye kuchinja siku hiyo husamehewa dhambi zake na jamaa zake
Na mwenye kumpa chakula maskini au akatoa sadaka Allah (SWT) atamfufua siku ya Qiyyammah kwa amali nzuri na mizani nzito ya thawabu zake zenye kushinda mlima "UHUD"
..
Tuesday, 22 August 2017
Mahojiano
No comments:
Post a Comment