Akizungumza na wanahabari jana kwa niaba ya wenzake 14, Mwenyekiti wa serikali ya Mitaa wa Keko Mwanga B, Shilingi Shilingi wanaunga mkono uamuzi wote wa Baraza Kuu la Uongozi kwa kuwa wabunge hao wamebainika kukihujumu chama hicho.
“Tunamtambua Maalim Seif Sharif Hamad kama katibu mkuu lakini kwa sasa nafasi yake inakaimiwa na Magadalena Sakaya kutoka na yeye kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya CUF,” alisema Shilingi
Wabunge waliotimuliwa CUF ni Raisa Abdallah Mussa, Khadija Salum Ally, Halima Ali Mohamed, Salma Mohamed Mwasa, Miza Bakari Haji, Riziki Shahari Mngwali, Saumu Heri Sakala na Severina Mwijage
No comments:
Post a Comment