Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel
akiwasiliasha mada kuhusu Ubunifu,Masoko na Ujasuliamali wakati wa
mkutano Mkuu wa Bodi ya Wakandarasi (ERB) Ukumbi wa Jakaya Kikwete
Convertion Center leo Mjini Dodoma.
Wajumbe wa Mkutano wa mkuu wa
Bodi ya Wakandarasi (ERB) wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo
pichani) alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu Ubunifu,Masoko na
Ujasuliamali katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convertion Center leo
Mjini Dodoma. Picha na Lorietha Laurence-WHUSM.
………………………………………………………………………..
Na Lorietha Laurence-WHUSM, Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amewataka
Wakandarasi nchini kutumia vyombo vya habari katika kutangaza ufanisi na
ubunifu wanaoufanya ili kupata soko kwa urahisi.
Prof. Elisante ameyasema hayo leo
Mjini Dodoma alipokuwa akiwasilisha mada ya kuhusu Ubunifu, Masoko na
Ujasiriamali katika mkutano Mkuu wa Bodi ya Wakandarasi nchini ambao
hufanyika mara moja kila mwaka.
“Wakandarasi ni watu muhimu sana
katika jamii yetu maana wamekuwa wakituvusha kutoka hatua moja kwenda
nyingine ikiwemo ujenzi wa miundo mbinu ya barabara, maji na
mawasiliano. Hivyo, ni muhimu kwenu kushirikiana na vyombo vya habari
katika kueleza mafanikio hayo” amesema Prof. Elisante
Prof. Elisante aliongeza kuwa
vyombo vya habari ni njia rahisi na ya haraka ya kufikisha ujumbe kwa
jamii katika kile kinachofanywa na watu wake hivyo ni budi wahandisi
kufanya kazi na waandishi wa habari katika kueleza yale waliyofanikisha.
Aidha, Prof. Elisante amewataka
wakandarasi hao kutumia fursa ya ujasiriamali, ubunifu na masoko katika
kuhakikisha bidhaa zao zinapata soko na kuuzwa kwa wingi ndani na nje ya
nchi ili kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujmla.
No comments:
Post a Comment