Wananchi wa mtaa wa Station kata
ya Mtakuja Halmashauri ya Mji Geita katika foleni wakisubiri kusajiliwa
Vitambulisho vya Taifa, wakati wa zoezi la usajili linaloendelea mkoani
humo.
Wananchi kata ya Bulela
Halmashauri ya Mji Geita wakisubiri huduma ya usajili wakati wa zoezi la
usajili wa Vitambulisho vya Taifa linaloendelea Mkoani Geita.
Wananchi kata ya Bulela
Halmashauri ya Mji Geita wakisubiri huduma ya usajili wakati wa zoezi la
usajili wa Vitambulisho vya Taifa linaloendelea Mkoani Geita.
Afisa Msajili Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa, akiendelea na zoezi la usajili Vitambulisho vya
Taifa kwa Wananchi wa mtaa wa Station kata ya Mtakuja Halmashauri ya Mji
Geita.
Maafisa wa Mamlaka ya Vitambulisho
vya Taifa wakiendelea na zoezi la uingizaji wa taarifa za wananchi
katika zoezi la usajili Vitambulisho vya Taifa linaloendelea katika
Halmashauri ya Mji Geita Mkoani Geita.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uratibu
Ofisi za wilaya Bi. Rehema Kionaumela akitoa maelekeza kwa Maafisa wa
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Mkoani Geita kuhusu taratibu
mbalimbali wakati wa maandalizi ya zoezi la usajili wa Vitambulisho vya
Taifa kwa wananchi wa Halmashauri ya Mji Geita.
……………..
Wananchi wa Halmashauri ya mji
Geita, mkoani Geita wameendelea kujitokeza kwa wingi kushiriki katika
zoezi la usajili na utambuzi linaloendeshwa na Mamlaka ya Vitambulisho
vya Taifa. Zoezi hili ambalo kwa sasa linaendelea mikoa yote ya Kanda ya
Ziwa na Kaskazini limekuwa ni fursa nzuri na muhimu kwa wananchi
kusajiliwa na kuwezeshwa kushiriki katika shughuli za maendeleo kutokana
na umuhimu wa taarifa zinazokusanywa.
Pindi mfumo huu utakapokamilika
wananchi watawezeshwa kupata huduma mbalimbali kwa urahisi pamoja na
kusaidia Serikali kuimarisha Ulinzi na Usalama wa nchi kwani
Kitambulisho hiki kitakuwa ufunguo kwa mifumo mingine ya Serikali
kubadilishana taarifa.
No comments:
Post a Comment