Jumla
ya kiasi cha sh,99 bilioni zinatarajia kugharamia ujenzi wa kiwanda cha
kisasa cha kutengeneza dawa za kufubaza virusi vya ukimwi(Arv”s)
kinachotarajia kujengwa jijini Arusha.
Kiwanda
hicho kinatarajia kuanza kujengwa mwishoni mwa mwezi huu ambapo
kitazalisha jumla ya dawa 500,000 za kufubaza virusi vya ukimwi kwa
mwezi na kuwafikia waathirika wa ukimwi milioni moja na nusu nchini kati
ya milioni 3 ambao wanaishi na maambukizi nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini hapa afisa mtendaji mkuu wa kiwanda
cha kutengeneza dawa nchini(TPH),Ramdhan Madabida alisema kwamba ujenzi
wa kiwanda hicho utasaidia kuokoa kiasi cha sh,806 bilioni kwa mwaka
zinazotumika serikalini kuagiza dawa nje ya nchi.
Madabida,alisema
kwamba fedha za ujenzi wa kiwanda hicho zimetokana na ufadhili
walioupata kutoka jumuiya ya umoja wa nchi za Ulaya(EU) ambapo
zitatumika katika awamu tatu ambazo ni ukarabati wa majengo,kutengeneza
mashine sanjari na kufanya upanuzi wa kiwanda.
Alisema
kwamba wao kama wawekezaji wa ndani wameamua kuunga mkono kauli mbiu
ya Rais John Magufuli kuhusu Tanzania ya viwanda na hivyo wamejipanga
kutoa ajira kwa vijana nchini zipatazo 200 kwa awamu ya kwanza.
“Mheshimiwa
Rais Magufuli ametutia moyo na tuna imani ametupa msukumo sisi
tutaendelea na uzalishaji na sio dawa tu pia tutazalisha malighafi na
sio dawa pekee”alisema Madabida
Madabida,aliwaambia
waandishi wa habari ya kwamba ujenzi wa kiwanda hicho utaendana sanjari
na ujenzi wa maabara ya kisasa ya utafiti na maendeleo kwa ajili ya
kuboresha utengenezaji wa dawa bora na kukifanya kiwe kitivo cha kutoa
taaluma kwa wanataaluma mbalimbali nchini.
Alisema
kwamba mashine zote katika kiwanda hicho zitaendeshwa katika teknolojia
ya hali ya juu kupitia mfumo wa kompyuta ambapo mbali na kutengeneza
dawa hizo za kufubaza virusi vya ukimwi pia kitazalisha dawa za kutibu
magonjwa ya vifua,malaria,tumbo sanjari na dawa zilizo kwenye orodha ya
dawa muhimu nchini.
“Kuanzia
mwaka 2018 tutawekeza katika kuongeza dhana za uzalishaji katika
kutengeneza dawa za sindano pamoja na dripu”alisema Madabida
No comments:
Post a Comment