
Akizungumza na Mo7news Online, DC Mjema,
amesema maadili ya watoto yameangamia kutokana na wazazi
kutojishughulisha na watoto zao kitu kinachozidi kuchangia mmomonyoko wa
maadili.
Aidha, DC Mjema amewataka wakina mama
kushika njia iliyo njema katika kufanya yale mema ambayo Mwenyezi Mungu
ameyataka na uacha yale ambayo yamekatazwa.
Hayo ameyasema kwenye ufunguzi wa
maulidi upande wakina mama, yaliyofanyika shule ya Msingi Muhibmbili
akta ya Tambaza Jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapata mualiko huo
wa kua mgeni rasmi.
"Wazazi kaeni na watoto zenu kurejesha
maadili, kama mtoto anakosea wewe uwe wa kwanza kumuadabisha, kama sisi
tukishindwa tunatengeneza kizazi sumu ambacho kitaleta matokeo hasi
ndani ya Taifa eltu tunapoelekea Tanzania Mpya ya Viwanda".Amesema DC
Mjema
Pia amesema ni jukumu la mzazi kujua
mtoto wake anafanya nini hata kama yupo masomoni nje au ndani ya nchi
anawajibu wa kujua maendeleo yake kwa ujumla ya kila siku na kufuatilia
mienendo yake ili kubaini mapungufu na ubora wa watoto zao.
Amesema kuwa kama Wazazi watalibebea
vyema jukumu la kuangalia Vijana wao katika upande wa maadili
watatengeneza kizazi kipya chenye maadili kitakachofuata misingi ya
dini .
Hata hivyo , DC Mjema , amewataka wazazi
mwakani watoe takwimu ya watoto waliowarejesha kwenye maadili mema ili
kuona ni changamoto gani wanazokabiliana nazo na kuzichukulia hatua.
No comments:
Post a Comment