Mbunge wa Jimbo la arumeru Mashariki Joshua Nassari, amevamiwa na watu
wasiojulikana nyumbani kwake Usa River mkoani Arusha, na kunusurika
kupigwa na risasi ambazo zimeua mbwa wake.
Kwenye
ukurasa wake wa twitter Joshua Nassari ameandika ujumbe akitoa taarifa
kuwa watu hao walivamia nyumbani kwake usiku wakiwa na silaha za moto
ambazo waliwafyatulia mbwa wake, na yeye kunusurika baada ya kukimbia
akiwa na mkewe, kitendo ambacho amesema kimemfanya akose imani na nchi
yake.
"Nimevamiwa nyumbani kwangu maeneo ya Usa River usiku huu na watu wenye silaha, na kufyatua risasi ambazo zimeua mbwa waliokuwepo nje ya nyumba. Nimefanikiwa kukimbia na mke wangu na kuripoti kituo cha Polisi. Nimekuwa nikitishiwa kuuawa kila siku, sina amani ndani ya nchi yangu", ameandika Joshua Nassari.
Kufuatia tukio hilo East Africa Television ilifanya jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha kupata taarifa zaidi juu ya tukio hilo, na simu yake kuita bila mafanikio.

Alichokiandika Joshua Nassari twitter
Mbwa wa Joshua Nassari ambaye alipigwa risasi
No comments:
Post a Comment