Akizungumza na Mo7news online, Mratibu
wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Manispaa ya Ilala, Martin
Kalongolela , amesema lengo la zoezi hilo ni kutoa kinga kwa Wanachi juu
ya magonjwa hayo ambayo yanahatari kubwa kwa Taifa.
Aidha, Kalongolela, amesema kuwa mpaka
sasa wana jumla ya vituo 159 vinavyo ratibu zoezi hilo la upimaji
ikiwemo, Serikali za Mtaa, Vituo vya mama na Mtoto, Masokoni, kwenye
mikusanyiko ya watu, Vituo vya mabasi ya kawaida na Mwendo kasi, pamoja
na Shule za Msingi.
Kalongolela, amesema lengo la kutawanya
vituo hivyo ni kuhakikisha wanawafikia wananchi wote walioko Wilaya ya
Ilala ili kujikinga na maradhi hayo.
Mratibu huyo, amesema zoezi hili
lisiishie kwa Wanaume peke yao bali hata wanawake linawahusu kwa kuondoa
dhana ya kuwa na busha na kuweka dhana ya kupata Matende ya matiti,
Matende ya miguu kwani mbu huyo hushambulia vifigo ambapo moja kwa moja
huathiri sehemu za siri.
Hata hivyo, Kalongolela, ametoa wito na
kuwataka Wanawake wajitokeze kwa wingi ili kujikinga na maradhi hayo
ambapo kwa mawanamke ni vigumu kuonekana tofauti na mwanaume.
Inakisiwa watu Milioni 120 duniani wana
maambukizi ya Matende , ambapo kati ya milioni 40 wamepata madhara
makubwa kutokana na ugonjwa huo.
Anasema zipo dhana mbali mbali kuhusu
ugonjwa wa Matende na Busha ambapo baadhi a watu wanadai unasababihswa
na kunywa maji ya madafu
“Dhana hizi si za kweli , matende na mabusha hayasababishwina maji ya madafu bali mbua aina ya Culex”. Amesema Kalongolela
Amewata wananchi kulala kwenye neti
safi na salama zilizowekwa dawa , huku akisema waliopata chanjo hiyo
mwaka jana ni Milioni moja na laki mbili sawa na 88% hivyo kusudio la
mwaka ujao ni kuwa na sehemu kubwa ya wapimaji wa chanjo hiyo.
No comments:
Post a Comment