• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday 21 December 2017

    Utawala bora,uwajibikaji,uwazi pamoja umoja imeelezwa kuwa itasaidia kukua Kwa Biashara ya utalii nchini.

    Image result for japhet hasunga 
    Na Stahmil Mohamed
    Haya yamezungumzwa Leo Naibu Waziri Wa maliasili na utalii  Mhe.Japhet Asunga alipokuwa akizindua vyombo vya  kusimamia Biashara ya utalii nchini ambapo ameitaka bodi ya utalii kushirikiana na kamati ya ushauri ,mamlaka ya rufaa kufanya kazi Kwa weledi na kuzingatia uwazi na uwajibikaji ili kuzidi kukuza uchumi Wa nchi kipitia sekta hii ya utalii kwakuwa ni sekta pekee ambayo inaitangaza nchi mahala popote hivyo kama haitazingatia misingi hiyo ya utawala bora tutazidi kuwavutia watalii zaidi na wataongezeka hivyo pato LA nchi litazidi kukuwa.
    Akivitaja vyombo vilivyozinduliwa Leo Mhe.Asunga amevitaja ni pamoja na bodi ya leseni ambayo itakuwa inatoa leseni Kwa wafanyabiashara Wa utalii pamoja na kufanya tathimini ya leseni,kamati ya ushauri ambayo itakuwa inaishauri bodi ya utalii hali ya Biashara inavoenda na mambo mengine,pamoja na Mamlaka ya rufaa ambayo itakuwa inashughulikia mambo ya sheria na rufaa zote hivyo yeye kama waziri anaamini kupitia
    vyombo hivo sekta ya utalii itazidi kuimarika na kuzidi kukuza zaidi pato LA nchi.

    Kwa upande Wake Mwenyekiti Wa kamati ya Ushauri Prof.Wineaster Anderson amesema sekta ya utalii ni sekta ambayo inachangia pato LA nchi kwa 18% inaajira 1200 na ajira za mmoja mmoja ni nusu bilioni hivo wao kama kamati ya ushauri itahakikisha inaishauri vizuri bodi ili ilizidi kukuza pato LA nchi zaidi.

    Naye Mwenyekiti wa kamati ya rufaa Mwanaidi Sinare Maajar amesema  kupitia kamati yao inafanya kazi Kwa wazi,haki pasipokugonganisha maslahi pia itahakikisha kunakuwa na taratibu za wazi ili watu wazijue vizuri ili kusitokea makosa ya Mara Kwa Mara.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI