Na Stahmili Mohammed.
Jumuiya
ya Chuo kikuu cha Dar es salaam (DARUSO)imewataka Vijana kuacha kuwa
wafia siasa na kuwa wazalendo ili kulisaidia Taifa lizidi kukua kiuchumi
hasa katika Kipindi hiki ambacho nchi inaelekea katika uchumi wa
Viwanda.
Haya
yamezungumzwa na Rais wa Chuo kikuu cha Dar es salaam Jeremiah John
Jilili alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema
kumekuwa na dhana kwa vijana ya kulowea kwenye siasa na kulalamika
pasipokufanya utafiti hali ambayo inalirudisha nyuma Taifa ambalo kwa
Sasa linaelekea katika uchumi wa kati wa Viwanda hivyo waachane na dhana
ya malalamiko.
Aidha
Jilili amesema kupitia mijadala ,midahalo mbalimbali amegundua na
kujiridhisha kuwa vijana wengi wa kitanzania wanauelewa mkubwa mpana na
takwimu sahihi za masuala ya nchi yetu lakini wanayumbishwa na mambo ya
kiitikadi kitu ambacho tukiwa wazalendo hayana tija kwenye Taifa letu.
Pia
Jilili amewahasa vijana kubadilika na kusema kuwa vijana ndio chachu
kubwa ya mabadiliko na maendeleo kwenye nchi yoyote ile duniani.
"Vijana tunatakiwa tubadilike kwani vijana ndio chachu ya maendeleo kwenye nchi yoyote ile duniani" amesema Jilili.
Sambamba
na hayo Jilili amempongeza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.
John Pombe Magufuri kwa kuwa mzalendo na kuendelea kusimamia matumizi
mazuri ya rasilimali za nchi.
"Tunampongeza Rais kwa kuwa mzalendo na kuendelea kudhibiti matumizi mabaya ya rasilimali za nchi"amesema Jilili.
No comments:
Post a Comment