Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jafo amevitaka vituo vyote vya Afya Nchini pamoja na hospitali
za Wilaya kutengeneza bustani za kupumzikia wagonjwa wanaosubiria
matibabu.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akikagua Ujenzi wa miundombinu ya Afya katika Kituo cha Afya Makole kilichopo Manispaa ya Dodoma na kuutaka uongozi wa Kituo hicho kutenegenza bustani ya kisasa pamoja na kupanda miti ya kutosha ili kutunza mazingira.

Kituo cha Afya Makole ni miongoni mwa vituo 211 Nchini vilivyopokea/vitakavyopokea fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya Afya kwa lengo la kuboresha miundombinu ya Afya
No comments:
Post a Comment