• Breaking News

    ..

    ..

    Friday 29 December 2017

    Waziri Mpango afunguka kuhusu deni la taifa

    Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imewatoa hofu wananchi kuhusu uvumi wa kuongezeka kwa deni la Taifa kwasababu deni hilo ni himilivu na liko chini ya ukomo wa hatari.
    Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam  na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philipo Mpango wakati akitoa mwenendo wa  hali ya uchumi na utekelezaji wa bajeti  ya Serikali kwa mwaka 2017/2018.
    Dkt. Mpango amesema katika tathimini iliyofanyika mwezi Novemba mwaka huu inaonesha kuwa uwiano wa deni hilo na pato la Taifa ni asilimia 32.5 likilinganishwa na ukomo wa asilimia 56.
    “Katika kuangalia ukomo wa deni hili ambao uko chini, inaonesha kuwa deni hili ni himilivu  katika kipindi cha muda wa kati na muda mrefu”, amesema Dkt. Mpango.

    Aidha Waziri Mpango ameongeza kuwa Serikali tangu ifanikiwe kuziba mianya ya rushwa na ufisadi imefanikiwa kukusanya trilioni 1.2 kila mwezi. Pia amewapongeza walipakodi nchini na kuwataka Watanzania kujenga tabia ya kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi.
    "Naipongeza Benki Kuu ya Tanzania kwa usimamizi mzuri wa Sera za Fedha, kuanzia Disemba 12 mwaka huu BOT imeshusha riba inayoitoza Serikali katika mikopo kutoka asilimia 6.5 hadi asilimia 3 ili kuchochea utoaji wa mikopo katika uchumi," amesema Dkt. Mpango

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI