• Breaking News

    ..

    ..

    Friday 29 December 2017

    Wizara ya fedha yatoa Mwenendo wa Hali ya uchumi na utekelezaji wa bajeti 2017/18

    Waziri Wa fedha na mipango mhe.Dkt Philip Mpango leo amekutana nawaandishi wa habari akiwa  lengo la kuwapatia watanzania taarifa rasmi kuhusu mwenendo wa uchumi wa taifa Kwa kipindi cha januari hadi juni 2017 na Kwa miezi ya hivi karibuni,utekelezaji wa bajeti ya serikali 2017/18 hadi Sasa na changamoto zilizopo mbele yao na matarajio mpaka juni 2018.                    

     Katika mwaka 2017(January-juni) Pato la taifa liliongezeka na kufikia shilingi milioni 25,535,852 ikiwa sawa na asilimia 6.8 huku ikilinganishwa na shilingi  milioni 23,915,750 katika kipindi cha mwaka 2016 ikiwa sawa na asilimia 7.7 huku akisisitiza  Kwa kusema Kasi chanya ya ukuaji wa uchumi inapungua na haimaanishi kuwa uchumi umeporomoka bali uchumi unaporomoka ukiwa katika kiwango cha hasi.                        

    Adha amesema ili Kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi iweze kuwanufaisha wananchi wengi wanatakiwa wawe wanafanyakazi katika sekta zinazokuwa haraka zikiwemo Ujenzi,habari na mawasiliano,usafirishaji na uhifadhi wa mizigo,uchimbaji wa madini na mawe, shughuli za fedha na bima.                      
    Sambamba na hayo Dkt.Philip Mpango amesema kufikia mwishoni mwa Septemba 2017 deni la taifa lilifikia shilingi bilioni 47,823.1 ikilinganishwa na bilioni 42,552.4 katika kipindi hiko cha mwaka 2016, ikiwa shilingi bilioni 13,417.5 ni deni la ndani sawa na asilimia 28.1 na shilingi bilioni 34,405.6 ni deni la nje ikiwa sawa na asilimia 71.9.              

    Hata hivyo amesisitiza kuwa ongezeko la deni la taifa lilitokana na kupatikana kwa mikopo mipya ya nje na ndani Kwa ajili ya kugharamia miradi ya Maendeleo ikiwemo ujenzi wa mradi wa umeme (kiwila coal mine) miradi ya uboreshaji wa huduma za maji,mradi wa kuzalisha umeme wa kinyerezi (150MW) na ujenzi wa ukarabati wa viwanja vya ndege.

    Kwa upande wa sekta za kibenki mwaka 2017  Waziri huyo amesema uligubikwa na kuongezeka Kwa mikopo chefuchefu kutoka asilimia 9.1 mwishoni mwa septemba 2016 hadi  12.5 septemba 2017  ikiwa juu ya wastani unaokubalika na Benki kuu wa asilimia 5 ,kupungua Kwa Kasi ya utoaji wa mikopo Kwa sekta binafsi na kupungua Kwa faida  itokanayo na uwekezaji kwenye rasilimali na mitaji.        
    Mbali na hayo Dkt.Philip  amesema matumizi ya fedha za kigeni sambamba na shilingi ya Tanzania hapa nchini linasimamishwa kwani wakati wa kufanya miamala mbalimbali yanaweza kuwa athari  kiuchumi ikiwa na kudhoofisha thamani ya shilingi.    

    "Sheria iliyopo Kwa Sasa haikatazi Jambo hili bali inasisitiza kuwa sarafu ya Tanzania ndiyo fedha halali na mtu au taasisi yoyote itakayokataa kupokea malipo Kwa shilingi ya Tanzania atachukuliwa hatua za kisheria." Amesema Dkt.philip Mpango                    
    Aidha serikali inaagiza kuanzia January mosi 2018  bei zote hapa nchini zitangazwe Kwa shilingi ya Tanzania,bei ambazo walengwa wake wakuu ni watalii au wateja wake Sio wakazi zinaweza kutangazwa Kwa fedha za kigeni na malipo Kwa fedha hizo za kigeni, mkazi yoyote wa Tanzania asilazimishwe kulipia bidhaa au huduma yoyote Kwa fedha za kigeni  na viwango vya kubadilisha fedha vitakavyotumika katika kuweka hizo bei katika sarafu mbili viwekwe wazi na visizidi vya soko.      

    Mwelekeo na matarajio yao hadi juni 2018 kuwa Kasi ya ukuaji wa uchumi wa mwaka 2017 unatarajiwa kufikia asilimia 7.0 ikitegemewa na uwekezaji mkubwa katika miundo mbinu hususani ujenzi wa reli mpya ya Kati  (SGR),bomba la mafuta kutoka Uganda,mradi wa umeme kinyerezi,ujenzi wa umeme striglers gorge, ujenzi wa barabara mbalimbali na uwekezaji wa sekta binafsi kwenye viwanda na huduma mbalimbali hususani utalii, biashara, usafirishaji mizigo kwenda nchi jirani na huduma za fedha.                          

    "Kipaumbele kukuu cha serikali ni kuendeleza kujenga uchumi wa viwanda ili kupanua fursa za ajira, kuboresha upatikanaji wa ubora wa huduma za jamii(maji,afya,e limu) na kupunguza umasikini" amesema Waziri huyo wa fedha na mipango.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI