• Breaking News

    ..

    ..

    Friday 29 December 2017

    Waziri Mkuu atoa agizo kwa TANESCO

    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtaka Meneja wa TANESCO wilaya ya Ruangwa, Bw. Samuel Pyuza kuhakisha umeme unapatikana mapema kwenye pampu ya maji ili kukamilisha mradi wa maji wa Namahema ‘A’.
    Majaliwa ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na wakazi wa vijiji vya Namahema ‘A’ na Namahema ‘B’ wilayani Ruangwa, mkoani Lindi, baada ya kukagua mradi wa maji ambao unatarajiwa kukamilika Januari 15, mwakani.
    Hadi kukamilika kwake mradi huo utagharimu Sh. milioni 244.52, na utahudumia wakazi 2,257 wa vijiji hivyo viwili ambao walikuwa wanasongamana kupata maji kutoka kwenye kisima ambacho kilikuwa kinatumia pampu ya mkono.

     Waziri Mkuu yuko kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka, lakini ameanza ziara fupi ya siku tatu, kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

    Jumla ya sh. milioni 189.93 zimeshatumika kwenye mradi huo ambazo ni sawa na asilimia 77.68 ya fedha ziliopangwa kutumika. Kijiji cha Namahema ‘A’ kina watu 1,668 na Namahema ‘B’ kina watu 589

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI