• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 25 January 2018

    MAVUNDE NA NDEJEMBI WAZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI MILIONI MOJA KONGWA

    Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti milioni moja katika kijiji cha Ibwagwa,Wilayani Kongwa Dodoma

    Mkuu wa wilaya ya Kongwa Deogratious Ndejembi akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti.

    Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde akipanda mti katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti milioni moja katika kijiji cha Ibwagwa,Wilayani Kongwa Dodoma.

    Mkuu wa wilaya ya Kongwa Deogratious Ndejembi akipanda mti katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti.
     
     wananchi wakishiriki upandaji miti Kongwa.
    Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde na Mkuu wa wilaya ya Kongwa Deogratious Ndejembi wakifurahi katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti.
     
     Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde  akiwa ameshika miche kwa ajili ya kupanda.


    Miti inayopandwa katika wilaya ya Kongwa
       …………………………………………………………………………….
     
    Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde
    leo amezindua kampeni ya upandaji miti milioni moja katika kijiji cha
    Ibwagwa,Wilayani Kongwa Dodoma ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya KIJANISHA
    DODOMA iliyozinduliwa na Mhe. Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.
     
    Waziri Mavunde amewataka wananchi wa Kongwa kuhakikisha
    wanatunza mazingira kwa kupanda miti mingi zaidi na kuwataka kuacha tabia ya
    kukata miti ambayo hali inayosababisha uharibifu wa mazingira mkubwa.
     
    Aidha Mavunde ametumia nafasi hiyo kuutaka uongozi wa Wilaya ya
    Kongwa kuhakikisha kwamba unasimamia utekelezaji wa sheria na kanuni mbalimbali
    za Mazingira ili kuinusuru wilaya hiyo na uharibifu wa Mazingira.

    Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mkuu wa Wilaya wa Kongwa Mhe.
    Deogratious Ndejembi amemuhakikishia Naibu Waziri Mavunde kwamba kama
    watahakikisha miti yote iliyopandwa inastawi ili kufikia lengo la kui-KIJANISHA
    DODOMA na pia ameahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote
    watakaobainika kuharibu mazingira hasa kwa ukataji miti na uchomaji wa misitu

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI