Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 17 Januari, 2018 amemteua Dkt. Titus Mwinuka kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Kabla ya uteuzi huu Dkt. Titus Mwinuka alikuwa akikaimu nafasi hiyo
Mnamo Januari 1, 2017 , Rais John Pombe Magufuli alitengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba na kumteua Dk Tito Esau Mwinuka kuwa Kaimu Mkurugenzi wa shirika hilo.
Kwa mwaka 2017 Mkurugenzi wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba alikuwa mfanyakazi wa kwanza kutumbuliwa na Rais John Pombe Magufuli

Dk Tito Esau Mwinuka Mkurugenzi mpya wa TANESCO
No comments:
Post a Comment