Halmashauri ya mji wa Mbinga mkoani Ruvuma imewafukuza kazi watumishi
wake 58 kwa makosa mbalimbali ikiwemo kughushi vyeti vya kidato cha nne
na wengine kwa kuisababishia hasara halmashauri hiyo.
Uamuzi
huo umetangazwa na Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Mbinga
Mheshimiwa Egno Kipwere ambapo watumishi waliofukuzwa kazi ni wa kada
mbalimbali wakiwemo walimu na Maofisa Watendaji pamoja na Afisa Misitu
wa halmashauri hiyo Bw. David Hyera.
No comments:
Post a Comment