Waziri Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikagua huduma za afya kwenye
kituo cha afya cha kamanga kilichopo Wilaya ya Sengerema.Waziri ummy
yupo Mkoani Mwanza katika ziara ya kikazi ya kujionea hali ya utoaji
huduma za afya mkoani hapo.
Waziri ummy Mwalimu akiangalia
ramani ya kituo hicho cha afya ambacho kimejengwa kwa ushirikiano wa
Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na Shirika la SEDA Foundation, kulia
ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.Subi na kushoto ni mmoja wa
Viongozi wa Shirika hilo.
Waziri Ummy Mwalimu akiangalia
Ramani ya Ujenzi wa jengo la ghorofa nne la Uzazi linalojengwa hospitali
ya Mkoa ya Sekoture jijini Mwanza.
.Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto akiangalia kazi inavyoendelea katika hospitali hiyo
Waziri Ummy Mwalimu na Naibu
Waziri Dkt.Angela Mabula wakikagua ujenzi wa jengo la dharura la uzazi
kwenye kituo cha afya cha Karume kilichopo kata ya Igombe Wialayani
Ilemela,akiyevaa koti la bluu ni Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt.Florian
Tinuga
Waziri Ummy Mwalimu akiangalia
duka la dawa lililopo kwenye hospitali ya Mkoa ya Sekoture ambapo
upatikanani wa dawa kwa Mkoa wa Mwanza ni asilimia 80.
Jengo la Maabara lililojengwa
kwenye kituo hicho cha afya katika mpango wa Serikali wa kuboresha
huduma za dharura za uzazi kwenye vituo vya afya nchini.(Picha zote na
Wizara ya Afya
No comments:
Post a Comment